June 8, 2016

Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu ameanza mazungumzo na Mbeya City na muda mchache ujao inaweza kumtangaza rasmi kuwa mchezaji wao.

Taarifa za ndani ya Mbeya City zinasema kwa asilimia kubwa, Kavumbagu raia wa Burundi na Mbeya City wamemalizana.

Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba amesema hawana tatizo kama Mbeya City na Azam FC wamemalizana.

“Hatjui kama wanazungumza na kama wanazungumza basi hakuna tatizo kwa kuwa mkataba wetu na Kavumbagu umebaki siku chache tu,” alisema.


Lakini mtu mwingine kutoka ndani ya Mbeya City amesema, klabu hiyo inatarajia kumtangaza Kavumbagu rasmi kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV