June 2, 2016


Vijana wetu, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeendelea na mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Misri.

Mechi hiyo ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Stars wanaonekana kuwa na matumaini makubwa na wengine wamekuwa wakiwashauri mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono hiyo Jumamosi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV