June 5, 2016


Mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Uhuru Selemani leo ameibukia katika michuano ya mchangani ya Ndondo Cup.

Uhuru ameonekana akiwa uwanjani akiitumikia timu ya Temeke Market  ambayo ilitoka sare ya bao 1-1  dhidi yaFaru Jeuri .

Bao la Faru lilipachikwa kimiani na Salum Kipanga ambaye anaicheza JKT Ruvu katika Ligi Kuu Bara huku lile la Temeke likipachikwa mkongwe na mtaalamu wa mchangani, Shaban Kisiga.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV