June 5, 2016Leo Juni 05, 2016 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekaa katika kikao chake cha kawaida cha 18.

Kamati ya Utendaji imepitia taarifa mbalimbali za ligi na kukubaliana namna ya kuboresha mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes, Ligi Daraja la Pili pamoja na Ligi ya Mabingwa wa Mkoa.

Kadhalika kamati iliangalia uendeshaji wa Ligi za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambayo wiki iliyopita ilipata udhamini wa haki za kuonyeshwa kwenye televisheni kutoka kituo cha televisheni cha Azam.

Pia Kamati ya Utendaji imepitisha azimio la kanuni ya leseni ya klabu kuwa ni lazima ianze kutumika msimu mpya wa mashindano wa 2016/17.

Mahitaji ya kanuni hiyo ni pamoja na klabu kuwa na Watendaji wa kuajiriwa kama vile Katibu Mkuu (GS), Mkurugenzi wa Ufundi (TD), Ofisa Usalama (Security Officer) na taarifa ya fedha zilizokaguliwa pamoja na Meneja wa Fedha ambaye atakuwa na uwezo wa kuandaa taarifa za fedha zitakazokaguliwa na wakaguzi wa mahesabu.

Pia klabu zinatakiwa kuwa na ofisi, Uwanja wa mazoezi, kuendeleza program ya vijana ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kusoma na  na kwamba hakuna mmiliki mmoja anayeruhusiwa kuwa na timu zaidi ya moja katika ligi.


Pamoja na hayo Kamati ya Utendaji iliteua wajumbe wa kamati mbalimbali za kawaida na za kisheria. Orodha kamili ya kamati hizo hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV