June 1, 2016Taifa Stars inashuka uwanjani Jumamosi hii ikiwa nyumbani kupambana na Misri katika mechi yake ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

Stars inahitaji ushindi kwenye Uwanja wa Taifa ambao ni uwanja wa nyumbani. Lazima ishinde ili kufufua matumaini ya kupata nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

Taifa Stars ni timu yetu sote, tayari Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premieum Lager wameonyesha uzalendo wa hali ya juu kabisa kuiunga mkono kwa kila kitu.

Sasa ni zamu yetu Watanzania kuungana nao na kuhakikisha Taifa Stars wanafanikiwa kuwatwanga Misri pale Taifa.

Kama utabaki nyumbani na kusema unaiunga mkono Taifa Stars hakika haitakuwa sahihi. Na kumbuka utakuwa unajidanganya.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam, Uwanja wa Taifa ni ndani ya jiji la Dar es Salaam. Lakini bado walio katika mikoa ya jirani wa nafasi ya kufika Uwanja wa Taifa ana kuiunga mkono timu yetu ya taifa.

Chonde chonde, kumbuka kubaki nyumbani, mwingine pia atabaki nyumbani. Twendeni tukaungane kuishangilia timu yetu hata kama mechi itaonekana kwenye runinga.

Hauwezi kuishangilia Taifa Stars ukiwa nyumbani, utakuwa unajidanganya. Hauwezi kuishangilia ukiwa unaangalia mechi kwenye kibanda. Twende pamoja uwanjani na kuwaunga mkono vijana wetu na tuwafunike Mafarano na mwisho, “wapigwe tu”.
.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV