June 30, 2016


Klabu ya Barcelona imeingia mkataba na kampuni ya Wapajapani ili kufanya marekebisho ya uwanja wake wa Nou Camp uwe na mwonekano mpya na kama hiyo haitoshi kuongeza idadi ya wanaoingia uwanjani kutoka watazamaji 90,000 waliokaa vitini hadi  105,000.

Kampuni ya Nikken Sennei Catalan inatarajia kuanza ujenzi huo mwaka 2017 kwa kitita cha pauni 465 na utamalizika mwaka 2021 lakini ujenzi utakuwa kwa awamu ili kuepusha kuathirika kwa ratiba ya mechi za nyumbani za Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV