June 18, 2016


Kuna uwezekano mkubwa beki mpya wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ akachezeshwa kesho Jumapili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, mwenyewe amesema akipata nafasi hiyo hatatoka kikosi cha kwanza.

Yanga kesho Jumapili inatarajiwa kucheza na MO Bejaia mechi ya Kundi A ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa l’Unite Maghrebine uliopo Bejaia, Algeria.
Dante aliyesajiliwa na Yanga siku chache zilizopita kutoka Mtibwa Sugar, ana nafasi kubwa ya kucheza katika beki ya kati na Kelvin Yondani kwani Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hayupo kikosini.

Cannavaro anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Sagrada Esperanca na Vincent Bossou ambaye hucheza nafasi hiyo, naye hakufanya mazoezi kikamilifu na wenzake kutokana na kuchelewa kujiunga nao.

Akizungumza kutoka Algeria, Dante alisema: “Kwa jinsi nilivyo fiti kutokana na mazoezi niliyofanya kambini Uturuki, naamini nikipata nafasi kikosi cha kwanza sitatoka.”

“Nitacheza kwa juhudi kubwa kumvutia kocha ili awe ananipa nafasi kila mara kikosini, labda nisipangwe lakini nikicheza tu nitahakikisha sikai benchi.”

Dante anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo mkabaji, alisema kambi ya muda iliyoweka Yanga nchini Uturuki tangu Jumapili iliyopita hadi jana Ijumaa, imewasaidia kwa kiasi kikubwa.

Mbali ya Dante, hadi sasa Yanga imewasajili Hassan Kessy kutoka Simba, Juma Mahadhi (Coastal Union) na Beno Kakolanya kutoka Prisons.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic