June 16, 2016


Kikosi cha Yanga, kipo tayari na kesho kinaondoka mjini Antalya kwenda Algeria kuivaa Mo Bejaia.

Yanga ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki kuingia katika hatua ya Kombe la Shirikisho katika hatua ya robo fainali.

"Kweli kikosi kinaondoka kesho kwenda Algeria tayari kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Mo Bejaia," alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Jerry Muro.

Yanga ilikuwa kambini Uturuki kwa siku tano kujiandaa na mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali itakayopigwa Jumapili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV