June 16, 2016Beki wa Yanga, Vicent Bossou ametua mjini Antalya nchini Uturuki na kuungana na wenzake.

Bossou ametua nchini humo katika kambi ya Yanga ambayo inatarajia kuondoka kesho kwenda Algeria kuivaa Mo Bejaia katika mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.


Beki huyo raia wa Togo alichelewa kujiunga na wenzake kutokana na matatizo ya kifamilia nchini Ivory Coast ambako ndiyo asili yake.

Alichofanya ni kuja hadi Dar es Salaam, halafu akaanza safari ya kwenda Antalya nchini Uturuki kuungana na wenzake na kesho ndiyo safari ya kwenda Algeria.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV