June 20, 2016Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, sasa wanarejea nyumbani moja kwa moja kuja kuanza maandalizi ya mechi inayofuata.

Awali Yanga ilitangaza kuweka kambi nchini Uturuki ili kujiandaa na mechi yake inayofuata ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Lakini Msemaji na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kikosi hicho kitawasili kesho nchini kikitokea nchini Algeria ambako kilikwenda kucheza dhidi ya Mo Bejaia na kupoteza kwa bao 1-0.

“Kikosi kitawasili kesho, tunaamini TP Mazembe ni timu bora lakini tuna uhakika wa mtaji mkubwa wa mashabiki na pia kikosi bora, tutapambana,” alisema Muro.


Kabla ya kucheza Algeria, Yanga iliweka kambi nchini Uturuki kwa siku tano na kufanya mazoezi ambayo huenda yalisaidia kwa kiasi kikubwa kiuchezaji kwani katika mechi dhidi ya Bejaia, Yanga ilionyesha soka safi lakini ikashindwa kuzitumia ili kupata mabao.

2 COMMENTS:

  1. wameghairi kwenda Uturuki tena! Koko koko tu hata akienda Ulaya atatafuta jalala!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV