June 20, 2016


MAGURI
Klabu ya Majimaji imepanga kujiweka sawa kweli kuhakikisha inaongeza mshambuliaji wa kuongeza nguvu ya mashambulizi na Elius Maguri ni kati ya waliomlenga.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Majimaji zinaeleza, tayari wameanza mazungumzo nna Maguri.

“Kweli kuna mazungumzo na Maguri, tunajaribu kuangalia ingawa alitueleza anaweza kucheza nje ya nchi.

“Lakini tunajaribu kuangalia kama tunaweza kuangalia kama inawezekana. Lengo letu ni kuimarisha kikosi,” kilieleza chanzo.


Majimaji chini ya Kocha Kally Ongala imefanikiwa kubaki Ligi Kuu Bara na uongozi umesisitiza, msimu ujao unataka kujenga kikosi imara zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV