June 1, 2016

BARAKA
Wakati Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ikitangaza kusogeza mbele zoezi la kuchukua fomu  za uchaguzi wa klabu ya Yanga mpaka Juni 5, mwaka huu, Uongozi wa klabu hiyo imeibuka na kutangza rasmi tarehe ya  uchaguzi huo ambao utafanyika Juni 11, mwaka huu.

  Kamati ya hiyo TFF iliyochini ya wakili, Allocey  Komba ilitangaza kuongeza siku za wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi huo kabla ya jana Jumatano, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja, kugilia msumari wa mwisho katika suala la uchukuaji fomu ambalo limeoneka kusususa.

 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deudiet alisema kuwa ameagizwa na kamati ya uchaguzi ya timu hiyo na bodia ya wadhamini kutangza tarehe rasmi ya uchaguzi huo ambayo  ni kinyume na ule uliotangazwa na TFF kwa madai ya kutokuwa na imani na waendeshaji wake.

 Deudiet alisema kuwa kamwe hawatoweza kukubali uchaguzi wao usimamiwe na watu ambao hawapo ndani ya timu yao ikiwa wao wanaendesha timu yao kwa kufuata misingi ya katiba huku wakishangazwa na kauli ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kuwa wahautambui uongozi uliopo madarakani.

“Nimepewa maelekezo ya na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na bodi ya wadhamini kutangaza mchakato wa uchaguzi wa klabu yetu kama tulivyotakiwa na serikali kufanya hivyo baada ya kuwaandikia TFF lakini tunashangazwa na TFF hao kutangaza mchakato  wa uchaguzi wetu ikinyume na inavyotakiwa.

 “TFF imetangaza uchaguzi utafanyika June 6 lakini sisi tutafanya June 11 mwaka huu  kwa kufuata taratibu zote baada ya kutangaza leo rasmi mchakato wa uchaguzi huo  kwa sababu ni jambo la kushangaza kwa mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa TFF, kusema kuwa uongozi wa Yanga ni batili.

 “Sasa kwa maana hiyo makombe yote matatu tuliochukua msimu huu ni batali na hata viongozi wetu ambao wanashiriki vikao halali vyote vya TFF nao ni batili, inashangaza kwa kweli  kusema hivyo wakati wao kupitia kwa katibu mkuu TFF wametuandikia barua ya kuomba fedha za kuendesha uchaguzi sasa wanawezaje kufanya hivyo ikiwa uongozi uliopo hawautambui?

“Lakini kwa nini TFF ing’ang’anie  uchaguzi wetu wafanye wao wakati Yanga ina wanachama wake na kamati zake ambazo zinahitaji zifanye mambo yake bila ya kuingiliwa na wengine hivyo tutafanya uchaguzi wetu kwa kama tulivyopanga wenyewe na wanachama wote ambao wanakadi zilizolipiwa zikiwemo zile za benki wana haki ya kupiga kura,” alisema Deudiet.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV