June 1, 2016


Hatimaye mshambuliaji nyota wa Real Madrid Karim Benzema amefunguka na kusema haamini kama Kocha Didier Deschamp amemuacha katika kikosi cha Ufaransa kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016 kwa uamuzi wake.

Benzema amesema aanamini kocha huyo na Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) walifanya hivyo kwa presha ya kisiasa na si kwa kupenda.

Awali gwiji la Ufaransa, Eric Cantona alimtupia dongo Deschamp kwamba aliwaacha Benzema na Hatem Ben Arfa kutokana na asili yao kuwa ni Kaskazini mwa bara la Afrika.

“Sidhani kama ni suala la ubaguzi lakini siamini kama walifanya hivyo kwa uamuzi wao, ni watu ambao sina uamuzi wao. Nafikiri ni presha ya kisiasa imewalazimisha kufanya hivyo.

“Nashangazwa na kusikia wachambuzi wa runinga wakisema sipendwi na watu, lakini kuna watu takribani milioni 40 wananiunga mkono mitandaoni,” alisema Benzema.


Pia kumekuwa na taarifa kwamba aliachwa baada ya ile kashfa ya suala la ngono iliyomhusisha mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena ambaye ilielezwa Benzema alimrekodi kwa makusudi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV