July 27, 2016


Katika kuhakikisha wanaziba nafasi ya mshambuliaji wao, Kipre Tchetche anayeusumbua uongozi wa Klabu ya Azam FC, mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba yupo nchini Ghana kumalizana na straika hatari wa timu ya Medeama FC, Kwame Boahene.

Licha ya Azam kujaza utitiri wa wachezaji wa kigeni ambao wanafanya majaribio ndani ya timu hiyo kwa sasa wakiwemo washambuliaji watatu, Mniger, Morsi Mussa Issa, Mzimbabwe, Bruce Kangwa na Ibrahima Fofana raia wa Ivory Coast.

Lakini wakaona ni bora kwenda kusaka straika mwingine kwa ajili ya kuziba pengo la Tchetche ambaye anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na moja ya timu za Oman.

Azam walianza kumfuatilia mshambuliaji huyo wakati Medeama ilipocheza na Yanga hapa nchini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, ambapo bosi huyo alifanikiwa kuzungumza na viongozi wa Medeama kabla ya kwenda kumuangalia tena katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga uliopigwa jana Jumanne huko Ghana.

Taaarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo, zinasema kuwa bosi huyo licha ya kumuangalia uwezo wake kwenye mchezo huo, lakini pia alipata nafasi ya kumshuhudia katika mazoezi ya mwisho yaliofanyika juzi Jumanne kabla ya mchezo huo wa jana na Yanga.

Ofisa habari wa  Azam FC, Jaffar Idd, amelithibitishia Championi Jumatano kuwa, Kawemba yupo nchini Ghana kwa ajili ya kumuangalia mchezaji huyo na wengine ili kuziba nafasi zenye upungufu.


“Ni kweli Kawemba yupo Ghana na amekwenda kuwaangalia wachezaji ambao kama mambo yakienda vizuri basi atarudi nao kwa ajili ya kuitumikia timu yetu, lakini pia akitoka huko atakwenda Ivory Coast kuangalia wachezaji wengine,” alisema Idd.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic