July 20, 2016Azam FC imeendelea na mechi mazoezi baada ya kuichapa Friends Rangers kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam inayonolewa na Zeben Hernandez raia wa Hispania, imeshinda mechi yake ya kirafiki baada ya kuanza kwa kuichapa Ashanti United kwa mabao 2-0.

Mabao ya Azam FC katika mechi ya leo, yamefungwa na nahodha John Bocco katika dakika ya 39 na Issa Mossi katika dakika ya 77 huku Cosmas Lewis akifunga bao pekee la Rangers katika dakika ya 90 baada ya kipa na mabeki wa Azam FC kutegeana.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV