July 20, 2016

CHUJI
Wachezaji wakongwe, Athumani Iddi ‘Chuji’ na Nizar Khalfan wametemwa katika kikosi cha Mwadui FC.

Pamoja na wawili hao, mshambuliaji Jerry Tegete na Razak Khalfan nao wametemwa katika kikosi hicho chini ya Kocha, Jamhuri Kihwelo maarufu kama Julio.

TEGETE (KUSHOTO)

“Kweli hatutakuwa nao kwa ajili ya msimu uliopita,” alisema Julio leo.

Hata hivyo, Julio alikataa kusema kama amewatema zaidi ya kusema amewapa nafasi ya wao kwenda kucheza kwingine.

RAZAK KHALFAN
“Ninawapa nafasi ya kwenda kucheza kwingine, nina wachezaji wengine ambao ni vijana zaidi ningependa kuwapa nafasi na wamekuwa wakinipa matumaini makubwa mazoezini,” aliongeza Julio.


Chuji, Tegete na Nizar walijiunga na Mwadui FC wakitokea Yanga na Razak alitokea Coastal Union ya Tanga na kujiunga na timu hiyo ya mkoani Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV