July 12, 2016

KAKOLANYA AKIWA MAZOEZINI YANGA.

Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali anaamini kipa mpya wa timu hiyo Beno Kakolanya atakuwa “nomaa”.

Pondamali ambaye ni mmoja wa makipa bora katika historia ya soka nchini, amesema Kakolanya ni mmoja wa makipa wazuri nchini lakini anapaswa kuongezewa mambo muhimu.

“Tunaendelea na mazoezi, Kakolanya ni kipa mzuri lakini bado kuna mambo ya kumuongezea. Yanga ni level nyingine hivyo lazima watu wakubali kwamba akiiva ni kipa hasa,” alisema.

Kakolanya amejiunga na Yanga akitokea Prisons ya Mbeya ambayo aliidakia kwa ubora wa juu na kuisaidia kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya nne.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV