July 27, 2016


Kikosi cha Azam FC kimeendelea na mazoezi yake ya kujiandaa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2016-17.

Leo Jumatano mchana kilipofanya mazoezi ya viungo ndani ya bwawa la kuogelea kwenye Hoteli ya Mtoni Marine, ilipofikia timu hiyo.


Programu hiyo ilisimamiwa na Kocha Msaidizi wa Viungo wa Azam FC, Borges Pablo.

Wachezaji hao walionyesha kufurahishwa na kazi nzuri ya Pablo raia wa Hispania na kuifanya kwa ufasaha.

Azam FC imeweka kambi mjini Zanzibar na leo inatarajiwa kuanza kucheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhiid ya Kombaini ya Wilaya Mjini na itapigwa saa 2:30 usiku.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV