July 27, 2016
Kazi ya kuhakikisha beki Shomari Kapombe anarejea katika kiwango chake ndani ya kikosi cha Azam FC, si ndogo. Lakini Kocha Msaidizi wa Viungo wa Azam FC, Borges Pablo, amesema inawezekana.

Hermano ameendelea kupambana kuhakikisha Kapombe anakuwa vizuri na amekuwa akimpa mazoezi maalum ambayo kweli akiyazingatia, bila shaka anarejea haraka sana.Kapombe ambaye ni beki aliyefunga mabao nane ambayo ni mengi zaidi kuliko mabeki wengine, aliumia mwishoni mwa msimu na kulazimika kuumaliza msimu akiwa anatibiwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV