July 24, 2016


Kocha Joseph Omog wa Simba ametangaza kuahirisha kwanza mechi za kirafiki ambazo zilitarajia kuanza kuchezwa jana, lakini sasa muda wake atautumia kwa mambo mawili.

Kwanza ni kuona wachezaji wengine ambao wamejiunga na kikosi chake, lakini ataanza na kupanga mikakati mipya baada ya kukiona kikosi chake.

Taarifa zinaeleza, leo pia wachezaji wa Simba wanapumzishwa na kocha huyo atakuwa muda mwingi na msaidizi wake, Jackson Mayanga wakipanga mambo kadhaa muhimu.

Habari za ndani ya kambi ya Simba, zimeeleza kuwa kila kitu kimekwenda kwa mpangilio waliotaka.

“Ndiyo maana kocha anachotaka ni kuhakikisha tutakapoanza mechi za kirafiki, basi moja kwa moja anakuwa anmalizia tu,” kilieleza chanzo.


Awali, Omog aliomba mechi tatu na tayari uongozi ulimtafutia dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro mechi mbili, pia dhidi ya Polisi Moro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV