July 24, 2016



Kocha Mkuu mpya wa Simba, Joseph Omog amesema anataka soka la kitabuni lakini la malengo.

Omog raia wa Cameroon amewaambia hivyo wachezaji wake wakati wa mazoezi na kusisitiza sasa watatumia muda mwingi kuucheza mpira.

“Kocha kasema anataka soka la malengo, hatuwezi kuepuka kupiga pasi nyingi lakini ziwe ni zile zenye malengo ya kutekeleza jambo,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.

Simba imejichimbia mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi na Omog amekuwa akiendelea kuwafua wachezaji wake huku akipata nafasi ya kupanga kikosi. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic