July 26, 2016


Kikosi kizima cha Barcelona kipo nchini England kwa ajili ya maandalizi yake ya msimu mpya.

Kikosi hicho chini ya Luis Enrique, kinaongozwa na nyota wake kama Lionel Messi na Luis Suarez wakati kinamkosa Neymar ambaye yuko kwao Brazil akijiandaa kushiriki Michezo ya Olimpiki.

Kambi hiyo ya siku sita iliyo katika enero la St George's Park,  Burton-upon-Trent pia ni sehemu ya kujiandaa na mechi dhidi ya Celtic, mechi itakayopigwa mjini Dublin.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV