July 29, 2016Kikosi cha Yanga kimerejea jana nchini kwa mafungu kikitokea nchini Ghana kilipokuwa kimeenda kwa ajili ya mechi yake ya marudiano ya kimataifa ya kuwania Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya nchini humo.

Timu hiyo imerejea ikiwa na machungu kibao iliyoyapata baada ya kutandikwa mabao 3-1, Jumanne ya wiki hii hali iliyoifanya izidi kujiweka katika mazingira magumu ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hayo.

Hata hivyo mabeki wa kati wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani, wamejikuta katika wakati mgumu kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana.

Baadhi ya mashabiki walisikika wakiwatuhumu Cannavaro na Yondani kuwa waliifungisha timu hiyo huku wakidai kuwa endapo mechi hiyo angecheza, Mtogo, Vincent Bossou pengine hayo yote yasingetokea.

Mashabiki hao baada ya kuona kuwa maneno yao hayo hayatafika popote waliamua kumsubiri kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm ambaye aliwasasili katika ndege tofauti na wachezaji hao na kumtaka achukue hatua kali dhidi ya wachezaji hao.

Mara baada ya mashabiki hao kulalamika kwa Pluijim, kocha huyo alisema: “Nimewasikia na nitayafanyia kazi maoni yenu hayo kwani hata mimi hilo nililiona.”


Yanga inaburuza mkia katika kundi lake ambalo ipo na timu za TP Mazembe ya DR Congo, Medeama ya Ghana na MO Bejaia ya Algeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV