July 20, 2016


Wakati  beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy akiendelea kufanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo bila ya kujua ni siku gani ataitumikia, hali hiyo imeonekana kumuumiza roho na kujikuta akisema kuwa endapo sakata lake na Simba litaendelea hivyo basi yupo tayari kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima.

Kessy ambaye alijiunga na Yanga hivi karibuni anashindwa kuitumikia timu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa uongozi wa klabu hiyo haukuzingatia taratibu za usajili wakati ulipokuwa ukimsajili kutoka Simba.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Simba unataka Yanga ilipe Sh milioni 126, ili Kessy aweze kuitumikia vinginevyo hataitumikia klabu hiyo, jambo ambalo lilimfanya Kessy kwenda kuomba msaada kwa Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza), ili waweze kumsaidia kuhakikisha anapata kibali kutoka TFF, kitakachomwezesha kuitumikia timu hiyo mpya.


Kessy alisema mpaka sasa hakuna kilichofikiwa na kama hali hiyo itaendelea kama ilivyo sasa basi yupo tayari kukaa nje ya uwanja kwa msimu mzima.

“Suala langu bado linaendelea na mpaka sasa sijapata jibu lolote kutoka Sputanza hata hivyo kama itaendelea hivi basi nitasubiri mpaka litakapomalizika hata kama itakuwa ni kukaa nje msimu mzima mimi nitakaa.

“Kuhusu kiwango changu kushuka naamini hakitashuka kwa sababu nipo katika timu nzuri.

“Lakini pia  nipo chini ya kocha mzuri ambapo nitakuwa nafanya mazoezi kwa nguvu zangu zote mpaka hapo suala hili litakapomalizika,” alisema Kessy.


Wakati tukienda mitamboni jana, mmoja wa Katibu Msaidizi wa Sputanza, Abied Kasabalala amesema kuwa, leo wameitwa TFF kuzungumzia sakata hili la Kessy.

SOURCE: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Waandishi wa habari mnapaswa kuwasaidia wachezaji wetu kuifahamu na kuiheshimu mikataba ya timu zao,wachezaji wetu bado wana "utoto mwingi zaidi kuliko weledi wenyewe wa mchezo wa soka.Ipo wazi kuwa mchezaji anapokuwa amebakisha mkataba wa chini ya miezi sita,anaruhusiwa kufanya mazunguamzo na timu yoyote itakayoonesha shauku ya kuihitaji huduma yake.Kilichoruhusiwa hapa ni " mazungumzo"huku akisubiri ukomo wa mkataba wake,ndipo akamilishe taratibu zingine za kimikataba na klabu mpya.

    Kessy alifanya kinyume,huku akijuwa bado ana mkataba na Simba(haijalishi hata kama ulibakisha Dk.1),Kessy aliingia mkataba mpya na Yanga,aliambatana na timu Misri na alishiriki katika sherehe na shamrashamra za ubingwa wa yanga huku akijuwa kuwa bado mkataba wake na Simba haujaisha.Alianza kuvaa jezi za Yanga na kuambatana na timu Uturuki na kwingineko huku akijuwa bado mkataba wake na Simba haujafikia tamati.Katika hali hiyo ni nani wa kulaumiwa?

    Tujifunze kwa wenzetu,Pamoja na Ibrahimovich kuwa huru kujiunga na timu yoyote na kuwepo na tetesi nyingi za kuhitajiwa na ManU,bado hakufanya jambo lolote,alisubiri hadi siku ya Mwisho ya kumalizika kwa mkataba wake ndipo alikamilisha taratibu za kujiunga ManU.Hatukuwahi kumuona akiwa kwenye jezi za ManU,wala hakuenda kufanya maziezi na ManU,alisubiri hadi siku ya mwisho ndipo aliyafanya hayo.

    Sasa katika hali hiyo,mchezaji aliyetoroka Kambini na kuonekana akiwa ameambatana na timu pinzani huku akivaa jezi,akisafiri na kufanya mazoezi na timu ambayo hana mkataba nayo,huko si kuuvunja mkataba wake mwenyewe hata kama mkataba huo ulikuwa umebakisha sekunde moja kumalizika?

    Sputanza,TFF,Waandishi na wote wenye dhamana na soka la bongo,waelimisheni wachezaji wetu wajitambue,watambue taratibu na sheria zinazotawala mpira,kuwa na mkataba ulio chini ya miezi sita,hakumfanyi mchezaji adharau mkataba wake na kuanza kuambatana na timu nyingine huku akivaa jezi zake na kushiriki kushangilia ubingwa.Huo ni ulimbukeni,Kama sheria na taratibu zikifuatwa,sioni Yanga na Kessy watakavyokwepa kosa hili.Wawalipe tu Simba ili wabaki na mchezaji wao walioshiriki kuuvunja mkataba wake na mwajili wake(Simba).

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pamoja na hoja ulizojenga sio mbaya ni nzuri lakini hapo pia kuna kukomoana nadhani huyu mchezaji Simba walimfukuza ingawa si kimaandishi japo kwa mdomo na kutomlipa hata mshahara wake sasa utegemee nini afanye au aishi vipi bila ya kulipwa mshahara wake unakumbuka aliambiwa na Simba nanukuu"SIMBA SI YA BABA YAKO WALA YA MAMA YAKO" kisheria mkataba huvunjika hata kwa kauli tu au kutotimizwa masharit ya mkataba kama kutolipwa mshahara na mambo mengine nadhani ninachokiona mimi hapo kuna sera za ubabe na kukomoana tu Je angejiunga na timu kama ya Ndanda au Majimaji yangezuka haya yote pia?.

      Delete
    2. Simba hawakumfukuza,walimsimamisha kwa utovu wa nidhamu yeye akaibukia kwenye vyombo vya habari na kusema harudi tena Simba huku akijuwa fika kuwa Simba ndiyo mwajili wake.Kutokana na kususa huko ndipo viongozi wa Simba wakamjibu kuwa Simba si ya baba yake wala mama yake.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic