July 28, 2016


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema vijana wake wapya wamekuwa wakimfurahisha na kuzidi kumpa matumaini.

Julio amesema mwendo mzuri wa wachezaji hao wapya unampa matumaini kuwa atakuwa na kikosi bora zaidi cha ushindani, msimu ujao.

“Ushindani ndiyo jambo muhimu na kama unafanya kazi na watu wanaokuelewa, basi ujue ni dalili njema,” alisema Julio.

"Nawapongeza sana wachezaji waliokuwa msimu uliopita, walifanya kazi nzuri. Wanaoingia nao watakuwa na deni la kuonyesha wana mchango."


Julio alianza kuonyesha anahitaji mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada ya kuwatema wachezaji akadhaa wakongwe kama Athumani Iddi ‘Chuji’, Jerry Tegete, Nizar na Razak Khalfan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic