July 28, 2016


Kocha Zdravko Logarusic anarejea jijini Dar es Salaam, safari hii akiwa amepewa kazi ya kukipima kikosi cha Simba.

Logarusic maarufu kama Loga, anakuja nchini ndani ya siku chache akiwa ameongozana na kikosi chake cha Inter Club cha Angola.

Kikosi hicho kitapambana na Simba katika mechi ya Simba Day ambayo itapigwa Agosti 8, siku ambayo Simba itauwa inatimiza miaka 80.


Tayari Logarusic alikuwa amesema angetamani kukutana na Simba na kuwaonyesha kazi yake ilivyo bora.

Sasa Simba inanolewa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon na imejichimbia mjini Morogoro.

Chini ya kocha huyo, Simba imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi Morogoro iliyo daraja la kwanza na kuivurumisha kwa mabao 6-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic