July 18, 2016


Kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko amesema si kazi rahisi kubeba tuzo ukicheza soka katika ardhi ya ugenini.

Kamusoko raia wa Zimbabwe, ametwaa tuzo ya kuwa mwanasoka bora wa mwaka kwa wageni katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.


“Hiki si kitu kikubwa sana, nashukuru kwa kuwa si kitu rahisi kucheza kwenye ardhi ya ugenini na kuwa mwanasoka bora.

“Ninatoa pongezi kwa benchi la ufundi la Yanga na wachezaji wenzangu wote kutokana na walivyonisaidia hadi nimekuwa bora,” alisema.


Kiungo huyo amejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea FC Platnums ya Zimbabwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic