Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe amesema atafurahi kama atafanikiwa kuifikia idadi ya mabao yaliyofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein Daima.
Daima maarufu kama Mmachinga, alifunga mabao 26 katika msimu mmoja. Tambwe alifanikiwa kufikisha 21 msimu uliopita.
Wakati wa ukabidhiwaji wa tuzo, Mmachinga ambaye ni mchambuzi wa gazeti la Championi, ndiye alimkabidhi Tambwe tuzo hiyo.
“Ningefurahi sana kuwa mfungaji bora tena msimu ujao, ila najua ni lazima kujituma ili nifanikiwe tena.
“Kukuhusu rekodi yake (Mmachinga), nitajituma zaidi ili nikiwezekana niifikie au kuipita. Pia najua inahitajika kazi kubwa na hasa katika kujituma,” alisema Tambwe ambaye ni mtaratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment