July 26, 2016


Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez anaamini beki Shomari Kapombe atarejea katika ubora wake na kufanya yake.

Zeben raia wa Hispania, ndiye ameagiza Kapombe kuanza kupewa mazoezi bora chini ya kocha wa viungo wa Azam FC, zoezi ambalo limeanza.

“Inahitaji muda, pia ni uvumilivu lakini atarejea katika hali yake,” alisema.


Azam FC iko mjini Zanzibar ambako imeweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV