July 26, 2016



MPIRA UMEKWISHAAAA
Dk 90, Msuva anagongeana vizuri na Mahadhi na kuachia shuti kali kabisa, kipa anapangua na kuwa kona. Inachongwa, kipa Paul Aidoo anaokoa tena
Dk 83 hadi 88, inaonekana hakuna matumaini tena kwa Yanga kurudisha mabao hayo mawili. Zaidi MEdeama ndiyo wanashambulia zaidi
Dk 81, Medeama wanafanya shambulizi tena, lakini Eric Kwakwa aliyeingia anawahiwa na Cannavaro
DK 79 mpira hauna mabadiliko makubwa na Yanga hakuna mashambulizi makubwa wanayofanya langoni mwa Medeama
Dk 74, Yanga wanapoteza nafasi nzuri nyingine baada ya kipa wa Medeama kuuwahi mpira wa Tambwe aliyempa Ngoma
Dk 70, Yanga wanamtoa Juma Abdul aliyeumia nafasi yake inachukuliwa na Amissi TambweDk 64 Kwame anaingia vziuri na kupiga shuti lakini Dida anaokoa

Dk 58 sasa, Yanga wamezidiwa sana, ingawa Medeama wanaonekana kulinda sana, lakini mashambulizi yao ni hatari zaidi kwenye lango la Yanga
Dk 47, Yanga wanamuingiza Juma Mahadhi kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima
Dk 48, Yanga nao wanamtoa mfungaji wa bao la kwanza Dk 46, Kipindi  cha pili kimeanza kwa kasi na Yanga wanamtoa Yondani anaingia Dante

MAPUMZIKO:
Dk 44, Medeama wanapoteza nafasi nyingine tena na Yanga wanalazimika kuwa makini. 

Mechi inaonekana kuelemea zaidi upande wa Yanga ambayo beki yake imeshindwa kukaa vizuri.
GOOOOOO Dk 37, Abbas Mohammed anafunga bao tena kwa kichwa cha kurukia baada ya mabeki kuonekana wamezubaa kabisa
Dk 32, Medeama wanaonekana kuwa na kasi zaidi na Yanga wana makosa mengi hasa upande wa ulinzi
GOOOOOOO Dk 23, Msuva anaifungia Yanga bao kwa mkwaju wa penalti baada ya Chirwa kuangushwa ndani ya boksi

GOOOOOOO Dk 21, Abbas Mohammed, anaweka mpira kifuani na kufunga bao safi kabisa

Dk 9 hatari lakini Dida anafanya kazi ya ziada na kuudaka
Dk 8, Medeama wanapata penalti hapa baada ya Cannavaro kumuangusha Agyei. Anapiga Adede lakini Dida anadaka vizuri kabisa
GOOOOOO Dk 7, Moses anaifungia Medeama bao la mapema kabisa
Dk 4, Twite anafanya kazi ya ziada kuokoa mbele ya Enock Agyei


Mechi imeanza kwa kasi kila upande unashambulia ingawa inaonekana Medeama wameaza kwa kasi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic