Hatimaye Kocha Joseph Omog ameanza kukiona kikosi chake kikicheza mechi ya kwanza ya kirafiki na kushinda kwa mabao 6-0 dhidi ya Polisi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Biblia cha Highlands cha Morogoro, Simba walionyesha soka safi na la kuvutia.
Raia wa Ivory Coast, Fredric Blagnon ameanza vizuri kwa kupachika mabao mawili sawa na yale ya Ibrahim Ajib.
Wengine waliofunga mabao ni Abdi Banda na Mussa Kijiko.
Hiyo ni mechi ya kwanza ya Simba ya kirafiki na ya kwanza kupata ushindi mnono, jambo ambalo litainua morali zaidi ya Msimbazi.
Duh wamenunua hata mechi ya majaribio na timu ya daraja la kwanza.
ReplyDelete