July 25, 2016


Klabu ya Real Madrid ndiyo ghali, yenye kikosi ghali na mafanikio makubwa barani Ulaya.

Madrid maarufu kama Los Blancos imeteuliwa kuwa klabu bora zaidi kwa karne ya 20. Hii ni kwa mujibu wa fedha ambazo hutoa kununua wachezaji wanaoifanya kuwa ghali lakini mafanikio makubwa kupitia kura zilizopigwa kwenye mitandao mbalimbali mikubwa duniani.


Gazeti la Marca la Hispania, limeripoti hivyo kuhusiana na Madrid na kueleza kuwa Madrid ina kikosi chenye thamani ya euro milioni 783 ikiwa ni zaidi ya euro milioni 12 dhidi ya wapinzani wao Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV