July 25, 2016Kikosi cha Bin Slum Veterani, kilitoka sare ya 3-3 dhidi ya kile cha TFF Veterani katika mechi tamu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, jana. 

Nahodha wa Bin Slum Veterani, Nassor Bin Slum ndiye aliibuka kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa amefunga bao moja kwa mkwaju wa adhabu. Mengine katika kikosi chake yalifungwa na Mohammed Banka na Clement Kahabuka.

Haijajulikana kama kreti hilo liligawiwa, au zote 'alipiga' mwenyewe mchezaji bora wa mechi!


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV