July 29, 2016



Rasmi uongozi wa Simba umethibitisha kufuzu kwa kiungo wao, Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Mpumalanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Kiungo huyo, alikuwepo kwenye majaribio hayo kwa muda wa wiki mbili mara baada ya kuitwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo ikiwa ni mara yake ya pili kwenda kwenye majaribio nchini humo ambapo awali alikwenda katika timu ya Bidvest lakini hakufanikiwa.

Rais wa Simba, Evans Aveva, ameliambia gazeti hili kuwa Mkude amefuzu majaribio lakini kilichokwamisha ni maslahi ambayo alitakiwa kupewa.

Aveva, amesema wao walijiridhisha kumuachia Mkude lakini mchezaji mwenyewe ndiye aliyekataa kutokana na maslahi madogo ya mshahara na fedha za usajili ambazo alitakiwa kupewa.

“Mpumalanga imeshindwa yenyewe kutoa ofa nzuri itakayomshawishi Mkude na uongozi, hiyo ni baada ya kutangaza kutoa ofa ndogo ambayo mchezaji mwenyewe hakuridhishwa nayo kabla ya kuomba kurejea nchini.

“Kama uongozi tulitoa nafasi ya mchezaji mwenyewe kuridhia kwenda huko kwa ofa ndogo waliyoitoa, lakini mwenyewe akakataa, tunaheshimu maamuzi yake na kumuacha kurejea kwenye timu yake ya Simba.

“Ilikuwa ni ngumu Mkude kucheza soka huko kwa mshahara wa dola 1,500 (Sh milioni 3), kama unavyojua kuna kukatwa kodi huko, hivyo ameona ni bora akaendelea kulipwa mshahara anaoupata hapa wa shilingi milioni mbili,” alisema Aveva.


2 COMMENTS:

  1. Uamuzi aliofanya mchezaji huyu wa kukataa kulipwa Dola 1500 (Sh. milioni tatu na ushei) ukiangaliwa haraka haraka unaweza kuonekana ni sawa, lakini mimi nauona si sawa. Kwa kuwa kucheza ligi ya nyumbani na ugenini ni kitu tofauti. Kama hiyo timu inashiriki ligi kuu ya Afrika Kusini si sawa na kucheza hapa nyumbani kwani Afrika kusini ligi yake ni ya ushindani zaidi tofauti na hapa kwetu! Hata kama maslahi yangekuwa sawa lakini angepata faida kubwa kucheza nje. Huo ndiyo ulikuwa mlango wa kutokea. Wachezaji wetu bado utoto unawasumbua, kama wana watu wanaowashauri sidhani kama kweli ni washauri wanaotaka vijana wetu waendelee kama maamuzi yenyewe ni haya ... Tutasubiri sana Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Alikuwa anataka akalipwe dola 4500 kama Ngasa kwa umido tuu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic