July 29, 2016


Bilionea kijana, Mohammed Dewji amesema rafiki zake ambao ni wafanyabiashara wenzake walimuita mwendawazimu baada ya kusikia anataka kuwekeza kiasi cha Sh bilioni 20 kwenye klabu ya Simba.


Dewji ambaye ni mbunge mstaafu wa Singida Mjini amesema Sh bilioni 20 ni fedha nyingi na si kama ambavyo watu wanafikiria ndiyo maana wafanyabishara wanaweza kushangazwa na hilo.

"Lengo lango ni kuleta mabadiliko na baadaye mafanikio ndani ya Simba, haiwezekani kupata mafanikio bila ya kuwekeza," alisema akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Posta jijini Dar es Salam, leo.


Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.

"Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi.

"Baada ya kuwa umewekeza, baada ya hapo unaanza kuangalia njia za kufanya ili kuongeza mapato. Usajili, uwanja na mambo mengine yanahitaji fedha," alisema.

"Unajua kama nikiwekeza fedha hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.

2 COMMENTS:

  1. Mambo sasa yapo hadharani. Anachotaka Mo ni kuimiliki timu ya Simba. Itakuwa ni mali yake. Kutakuwa na wamiliki wengine wenye hisa ndogondogo lakini yeye andiyo atakuwa mwenye timu.
    Maana yake ataamua nani awe mtendaji pale Simba. Urais wa akina Aveva itakuwa bye bye. Wengine waliobaki watakuwa mashabiki sio wanachama wenye uwezo wa kuamua lolote.
    Wana Simba uamuzi ni wenu. Tajiri huyo kaja. Muuzieni hiyo bidhaa inayoitwa Simba Sports Club!

    ReplyDelete
    Replies
    1. muhimu ni simba iwepo,na kuna umuhimu gani wa Aveva kuwepo simba ikiwa hamna mafanikio..jambo ni moja tu timu inahitajki fetha ilikutatua matatizo ndani ya timu..ikiwa una pesa unaweza kununua mchezaj na kujenga uwanja...

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic