July 24, 2016 
Man United inashuka uwanjani kesho kuivaa Man City kwa mara ya kwanza nje ya ardhi ya England.

Lakini Kocha Jose Mourinho wa Man United amesema ana hofu kutokana na mvua mfululizo, hali inayoweza kusababisha majeraha kwa vijana wake kabla ya kuanza msimu mpya.


Timu hizo kutoka mji wa Manchester United, zinakutaka kesho kwenye uwanja wa Bird Nest maarufu kama Kichali.


Kumekuwa na mvua mfululizo karibu saa 24 bila kukatika na kusababisha hali ya uwanja kuwa mbaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV