July 26, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema hana hofu na hali ya hewa ya Ghana na haiwezi kuwasumbua kwa kuwa haina tofauti kubwa na ile ya Dar es Salaam.

Pluijm ambaye makazi yake yako nchini humo, amesema tayari kikosi chake kimekaa vizuri na wanaendelea vema na maandalizi.

“Siwezi kusema kuna kipya, mechi itakuwa ngumu kama nilivyosema mwanzo. Lakini tunataka kushinda na kama nilivyoeleza tulisharekebisha,” alisema.

Yanga iko nchini Ghana kwa ajili ya mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ambayo imepangwa kupigwa Leo saa 12 jioni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV