July 3, 2016Kocha wa Yanga, Hans va der Pluijm amekubali kwamba atalazimika kuongeza mambo kadhaa kwa mshambuliaji wake mpya Obey Chirwa.

Chirwa raia wa Zambia amejiunga na Yanga akitokea FC Platnums ya Zimbabwe na tayari amecheza mechi moja dhidi ya TP Mazembe.

“Ni mchezaji mzuri kama nilivyosema mwanzo, lakini lazima tuheshimu utaratibu wa mpira, kuna hatua.

“Suala la nguvu, pia kasi ni kati ya mambo tunayafanyia kazi, mfumo wa Yanga uko tofauti na timu nyingi,” alisema Pluijm.


Pluijm amesema, Chirwa ataenda anaimarika taratibu kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine ambao walijiunga na Yanga na si kweli kwamba wote walianza na viwango vya juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV