July 3, 2016


Tayari Yanga imepoteza mechi mbili za hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho na Kocha wake, Hans va der Pluijm amesema uzoefu umechangia.

Pluijm raia wa Uholanzi amesisitiza timu yake ilicheza vizuri katika mechi zote mbili dhidi ya Mo Bejaia ikiwa ugenini Algeria, pia TP Mazembe ikiwa Dar es Salaam na zote kupoteza kwa bao 1-0.

"Uzoefu ndiyo jambo lililotupa wakati mgumu kabisa. Tulipata shida kwa kuwa wenzetu wanakuwa tofauti kidogo na unajua uzoefu unasaidia sana.

"Hata Bejaia wana wachezaji ambao waliwahi kucheza michuano hiyo, lakini hili halitukatishi tamaa.

"Maana hakuna anayeweza kusema hatukuwa katika kiwango bora, lakini pia hatuwezi kukataa kwamba tulipoteza mechi zote mbili na ilikuwa muhimu kushinda au kupata pointi," alisema Pluijm.

"Bado hatujakata tamaa, tutaendelea kupambana zaidi. Tutajua katika mechi ya Medeama, nafikiri itatoa majibu."

Yanga iko mkiani katika kundi A linaloongozwa na TP Mazembe yenye pointi 6, inafuatiwa na Bejaia yenye 4, Medeama yenye moja na Yanga haina pointi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV