July 20, 2016


Baada ya kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe kupata tuzo ya mchezaji bora wa kigeni katika tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juzi , mchezaji huyo ametangaza vita katika msimu ujao wa ligi kuu.

Kamusoko aliibuka kinara wa mchezaji bora wa kigeni kwa kupata zawadi ya sh milioni 5, huku akiwapiku Donald Ngoma raia wa Zimbabwe pamoja na Vicent Angban wa Simba raia wa Ivory Coast.

Akizungumza jijini Dar, Kamusoko alisema anashukuru kwa ushirikiano alioupata msimu uliopita hadi kufikia kupata tuzo hiyo ya mchezaji bora wa kigeni, hivyo kwa sasa nguvu zake anazielekeza katika msimu ujao ili aweze kufanya vizuri zaidi.
“Nachukua nafasi hii kuwashukuru watu wote walionipa ushirikiano msimu uliopita, kwani ulikuwa ni msimu mzuri kwangu na timu yangu ya Yanga kwa ujumla kwa ushirikiano walionipa.

“Pia nawashukuru wadhamini ambao ni Vodacom kwa kunichagua mimi kuwa mchezaji bora wa kigeni na bila ya kuwasahau wote walionipa ushirikiano ndani ya Yanga, hivyo kwa sasa mtazamo wangu ni katika msimu ujao ili nifanye vizuri,” alisema Kamusoko.

Ukiachana na Kamusoko wachezaji wengine waliopata tuzo katika kikosi cha Yanga ni pamoja na Amissi Tambwe ambaye alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa msimu, Juma Abdul aliyepata tuzo ya mchezaji bora wa msimu pamoja na kocha wao Hans van Pluijm aliyepata tuzo ya kocha bora.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic