July 27, 2016Wakati Yanga ya Tanzania imepoteza matumaini kabisa ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, TP Mazembe, leo wamejihakikishia nafasi hiyo.

TP Mazembe imeilaza Mo Bejaia kwa bao 1-0 katika mechi iliyopigwa mjini Lubumbashi, mfungaji akiwa Rainford Kalaba katika dakika ya 61.

Kwa ushindi huo, Mazembe imefikisha pointi 10 ambazo zinaipa uhakika kubaki katika nafasi ya kwanza au ya pili kulingana na matokeo ya mechi mbili zilizobaki kwa kila timu ya Kundi A.

Bejaia wana mechi mbili, dhidi ya Yanga ugenini na Medeama nyumbani wakati TP Mazembe mbili zao, moja ni ugenini dhidi ya Medeama na nyumbani dhidi ya Yanga.

Kama itashinda mechi nyingine moja kati ya hizo mbili, TP Mazembe itakuwa imejihakikisha kukaa kileleni mwa kundi hilo.

Kwa muonekano, Mo Bejaia iliyo katika nafasi ya pili na Medeama nafasi ya tatu, kila moja ina nafasi kwa kuwa kila moja ina pointi tano.

Lakini uwezekano wa kufuzu unabaki kwa moja kwa kuwa zitakutaka. Kama zitatoka sare, zitakuwa zimeipa nafasi Mazembe kubaki kileleni lakini moja ikishinda, itakuwa imepata nafasi na moja kupoteza.

Bejaia watataka kushinda mechi dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam, ili mechi ya mwisho dhidi ya Medeama iwe fainali. Lakini Medeama nayo italazimika kuilaza Mazembe ugenini ili iwe isubiri mechi ya mwisho.

Kwa kifupi, sasa ushindani wa nafasi moja umebaki kwa Bejaia na Medeama huku Yanga ikiwa imeaga rasmi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV