July 23, 2016


Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Didier Kavumbagu huenda akakaa nje ya uwanja kwa nusu msimu baada ya timu ya Dong Tan 
Long ya Vietnam iliyotangaza kumsajili, kuahirisha.

Timu hiyo maarufu kama DT Long amebadili gia angani na kumsajili mshambuliaji mwingine raia wa Nigeria, siku chache tu baada ya kumsajili Kavumbagu.

Kutokana na kubanwa na nafasi za wachezaji wa kifeni, DT Long iliamua kumuachia Kavumbagu aende licha ya kuwa imeshampa fedha.

Lakini tatizo limekuwa ni kwenye ITC (uhamisho wa kimataifa) kwa kuwa tayari ilishapewa. Sheria za Fifa zinaagiza mchezaji angalau kuitumikia timu hata nusu msimu au msimu mmoja kabla ya kuhama tena. Hawezi kuhama bila kucheza hata nusu msimu halafu akahama tena.

Kuhusiana na hilo, Kavumbagu alisema: “Nilifanya majaribio katika timu ya Dong Tan nikafuzu, ajabu wakamsajili mchezaji kutoka Nigeria, nami nikaenda timu nyingine. Sasa Dong walikuwa wameshapewa ITC yangu.


“Ikaonekana kama nimesajili timu mbili lakini haikuwa hivyo, meneja wangu alikasirika sana ila Dong nao wanaona kama wametumia fedha zao bure kwangu, ila mambo yanaenda sawa naweza kucheza Oktoba ligi mpya itakapoanza.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic