July 23, 2016

ZEBEN AKIWA NA MSAIDIZI WAKE
Kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez amesema ameshangazwa na taarifa za yeye kutaka kumuacha John Bocco.

Zeben raia wa Hispania amesema ameshangazwa na taarifa hizo kwa kuwa hakuwa kusema suala hilo.

"Sijui walipolitoa jambo hilo, lakini si kweli na Bocco ni kati ya wachezaji mfano nimewakuta hapa na anafanya majukumu yake vizuri kabisa," alisema.

Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa kwamba Zeben na jopo la makocha kutoka Hispania wanataka kumuacha nahodha huyo wa Azam FC ambaye alianza kuichezea timu hiyo tokea madaraja ya chini.


1 COMMENTS:

  1. wakimuacha BOCCO wajiandae na mabegi yao kabisaaa...maana tuta andamana mpaka mlangoni kwa bakhresa

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV