Yanga inatarajia kuondoka nchini Jumamosi kwenda Accra, Ghana kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ya Ghana.
Wakati inakwenda Ghana, Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm itamkosa beki wake wa kati, Vicent Bossou raia wa Togo ambaye ameumia bega.
Pamoja na Bossou, Yanga itawakosa Dues Kaseke ambaye ameanza mazoezi jana baada ya kupata ajali ya pikipiki pia Geofrey Mwashiuya ambaye ni majeraha wa goti.
Bossou aliumia wakati Yanga ikipambana na Medeama katika mechi iliyochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika safari hiyo, Yanga itaondoka Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 21 kwenda Ghana.
0 COMMENTS:
Post a Comment