Kocha mpya wa Simba, Joseph Omog amepata mechi tatu za kirafiki ambazo ataanza kukiona kwa mara ya kwanza kikosi chake kikicheza mechi ya kirafiki.
Mechi ya kwanza ya kirafiki ya Simba itakuwa ni Jumamosi wakati watakapowavaa Burkina Faso ya Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapo.
Baada ya hapo, mechi ya pili imepangwa kuwa dhidi ya Polisi Morogoro kabla ya kurudiana na Burkina Faso tena, mechi inayoelezwa kuwa itapigwa nje ya mji wa Morogoro.
Simba chini ya kocha huyo raia wa Cameroon, imekuwa imejichimbia mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi na kocha alikuwa akiwafua wachezaji wake na sasa umekuwa ni wakati wake ambao anaamini ni mwafaka kuanza kuwapima kwa mechi.
0 COMMENTS:
Post a Comment