August 3, 2016



Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva amesema  kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ni wa kwao  katika mafanikio kwao huku akitamba kikosi chao kitakuwa tishio kama Medeama ya Ghana.

Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya kumaliza Mkutano na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Milenium Tower uliokuwepo Makumbusho Jijini Dar es Salaam.

Jeuri hiyo, huenda akaipata zaidi mara baada ya Mfanyabishahara mkubwa nchini, Mohamed Dewji kuahidi kuwekeza kwenye klabu hiyo ikiwemo kutoa fungu la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Aveva alisema hawaoni sababu yoyote ya wao kuukosa  Ubingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na mikakati wanayoendelea nayo ya kukiimarisha kikosi chao.

Aveva alisema, timu yao inaendelea na kambi yao ya pamoja chini ya Mcameroon, Joseph Omog na Mganda, Jackson kwa kuziimarisha sehemu mbalimbali, licha ya kocha wao huyo kuwathibitishia viongozi kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya ligi.

Aliongeza kuwa, wakati kocha huyo akiendelea kukiimarisha kikosi chake, bado anaendelea kuwaangalia wachezaji wa kimataifa waliokuwepo kwenye majaribio hayo akiwemo Janvier Bukungu, Mousa Ndusha (DR Kongo), Method Mwanjali (Zimbabwe) na Fedric Blagnon raia wa Ivory Coast.

"Kama uongozi kiukweli tumejidhatiti vya kutosha kuhakikisha mwaka huu unakuwa wa mafanikio kwenye klabu yetu, tunashukuru jitihada hizo tayari tumezianza kwa maana ya timu kuiweka kambi kwa muda mrefu.

"Tunajivunia benchi zuri linaloongozwa na Omog huku akiendelea kukiaandaa kikosi chake kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu ndani ya wakati mmoja akiendelea na zoezi zima la usajili kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu.


"Msimu uliopita uongozi tulishindwa kuuchukua ubingwa kutokana na matatizo ya hapa na pale ikiwemo usaliti wa wachezaji, lakini safari hatutakubali kutokana kwani tuna kikosi kilichokuwa imara na bora kitakacholeta ushindani wa ligi kama Medeama ya Ghana (waliowafunga Yanga Caf),"alisema Aveva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic