August 3, 2016

KIMWAGA WAKATI AKIITUMIKIA SIMBA
Kocha wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amevamia kwenye timu ya Azam baada ya kumtwaa kiungo mshambuliaji wake Joseph Kimwaga ambaye msimu uliopita aliitumikia Simba.

Kimwaga ametua Mwadui FC mara baada ya kutokuwemo kwenye mipango ya Kocha wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez ambapo kiungo huyo ametua kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, amesema kuwa wameamua kumpeleka kiungo huyo Mwadui kwa ajili ya kwenda kukuza kiwango chake kabla ya kurejeshwa kwa miaka ya baadaye pale atakapohitajika.

“Ni kweli Joseph Kimwaga hatakuwa na sisi kwenye ligi ijayo kwa sababu tumempeleka Mwadui kwa mkopo ambapo tumemwambia aende kukuza kiwango chake mara baada ya kocha kutomhitaji kwa sasa.


“Tumempa nafasi hiyo kwa kuwa yeye ni chipukizi na anahitaji muda zaidi wa kucheza, ndiyo maana tumempeleka huko lakini pia beki wetu Abdallah Kheri naye ametua African Lyon,” alisema Jaffar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV