August 26, 2016


Katika kuhakikisha inakuwa na kikosi bora siku zijazo, uongozi wa Klabu ya Azam umeanzisha mkakati wa kusaka vipaji vya vijana chini ya umri wa miaka 17 unaotarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, mwaka huu wakianza na Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd ambaye timu yake inaongozwa na nahodha John Bocco, amesema mpango umekamilika ingawa mpango mzima utaanza Agosti 28 wakianza na Wilaya za Kigamboni na Temeke kwenye Uwanja wa Chamazi.

Septemba 3, mwaka huu majaribio yatakuwa kwa Wilaya ya Ilala ambapo zoezi la ung’amuzi wa vipaji hivyo litakuwa kwenye Viwanja vya JMK kabla ya kuhamia kwenye Uwanja wa Kawe Septemba 10 kuhusisha Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuhamia katika mikoa mingine kama Zanzibar, Tanga, Morogoro, Arusha, Mwanza na Kigoma.


“Muhimu ni kila mzazi kuja na mwanaye siku ya kuwajaribu kwa ajili ya kupata taarifa za kina juu ya mtoto wake,” alisema Idd.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV