August 26, 2016

TEVERAS

Kocha wa African Lyon, Mreno, Bernardo Teveras, ameibuka na kusema kuwa anahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kuwa alishawaona walipocheza na Azam FC, hivi karibuni.

Mreno huyo amechukua nafasi ya kocha wa zamani wa Simba aliyekuwa akiinoa timu hiyo, Dragan Popadic raia wa Serbia aliyeondoka nchini kutokana na madai ya vyeti vyake kuwa ni vya kizamani na havifai katika soka la sasa.

Tavares amesema kuwa kwa sasa akili yake ameielekeza katika mchezo dhidi ya Yanga kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika ligi.

“Tulikuwa na wakati mzuri katika mchezo wetu dhidi ya Azam, japokuwa wapinzani wetu walipata nafasi ya kusawazisha dakika za mwisho, kwa sasa mipango yangu naielekeza katika mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga kwani nahitaji ushindi kutoka kwao.


"Uzuri ni kwamba Yanga tayari nimeshawaona walipocheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam kwani ni timu nzuri na ya gharama, lakini ninachokitaka ni ushindi pekee licha ya muda mchache ambao nimekaa nayo ila imani yangu ni kuwafunga tu, hakuna kingine," alisema Tavares.

African Lyon ilionyesha soka safi na kuibana Azam FC katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV