August 20, 2016


LICHA ya ubora wa picha angavu, bado Kampuni ya Azam TV imeona haitoshi na kuamua kuongeza vifaa vya kisasa zaidi pamoja na kufanyia marekebisho changamoto zote walizokumbana nazo msimu uliopita katika kurusha matangazo ya Ligi Kuu Bara.
Ikumbukwe kuwa Azam TV, wiki kadhaa iliingia mkataba wa miaka mitano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wenye thamani ya Sh bilioni 23 kwa ajili ya matangazo ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza leo Jumamosi katika viwanja tofauti.
 

Kaimu Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando, amesema kuelekea msimu mpya, wameboresha huduma zao ikiwemo gari la kisasa la matangazo (Ob Van), kila mechi kuwa na kamera si chini ya sita na kujenga majukwaa ya muda katika baadhi ya viwanja vyenye miundombinu mibovu ili kupata picha nzuri.
“Awali kuna baadhi ya viwanja tulipata shida sana ya kupata picha bora kutokana na miundombinu ya viwanja lakini hilo tumelikabili. Tumeongeza gari la Ob Van la kisasa na bora zaidi Afrika nzima, hivyo tunatarajia kuwa na picha zenye ubora wa hali ya juu,” alisema Mhando.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV